Thursday, January 5, 2017

SMITHMAI2016

Mwaka 2016 smithmai ilifanikiwa kutengeza bidhaa mbalimbali kama smithmaichill, kiongeza hamu ya kula, unga wa lishe, viungo vya chai na vingine ambavyo vinatumika kutengeneza pesa inayotumika kuendesha shughuli za za kutengeneza kipato kupitia vipaji mbalimbali kwa vijana wa kitanzania.
Pichani ni unga wa lishe, ambao unatumiwa kwa watoto, wanyonyeshao, watoto, wajawazito na familia kwa ujumla.
Pichani ni viungo vya chai, ambavyo vimetengenezwa kwa soya na vitunguu swaumu.

Hizo hapo juu zinaitwa #bryceson chocolates donats, zinatumika kama vitafunwa. Bidhaa hizi zimewezesha kutekeleza miradi ya vijana ya kujikwamua kiychumi kupitia vipaji, ambapo mpaka sasa tumeanzisha filamu, zinazochezwa na vijana wenye vipaji vya uigizajikama filamu ya penzibiashara na zingine.

Monday, July 11, 2016

#Smithmaiproducts


Mpaka kufikia tarehe 20/05/2016 Kampuni smithmai ilifanikiwa kubuni na kutengeneza bidhaa saba na hivyo kufanikisha lengo la mwaka 2015/2016
Bidhaa hizo ni, Smithmaishoes, Smithmaishibe, Chai smithmai, SmithmaiChill, Bryceson Donati, Maiken beauty na Wastara wine
Smithmai chill ni appetizer ya chakula inayotengenezwa kwa kutumia chillies

Watara Wine ni kinywaji kipya kisichokua na kilevi kinachotengenezwa na matunda asili, chenye ladha ya wine

#Smithmaiday2016

Smithmaiday, ni siku maalum kwaajili ya kuhamasisha vijana kujiajiri na kuondokana na utegemezi wa kiuchumi, hufanyika mara moja kwa mwaka kila tarehe 27 ya mwezi wa tano, ambapo watu mbalimbali hualikwa kuzungumza na vijana na makundi mengine ya watu nkuhusiana na kujiajiri, pichani ni mkurugenzi wa Munat Investment akizungumzia jinsi alivyoanza kufanya shughuli zake za utengenezaji mabegi ya wanawake
Siku ya smithmaiday 2016 Wajasiriamali mbalimbali walipata fursa ya kuzungumza namna wanavyoendesha shughuli zao, pichani ni mjasiriamali mdogo wa bidhaa za pilipili akizungumza machache kwenye Smithmaiday 2016
Licha ya idadi ndogo ya vijana, wachache waliokuwepo walipata firsa ya kujifunza na kuongea na washiriki wa tukio hili kuhusu fursa zilizopo kwenye sekta mbalimbali
Safari hii baadhi ya wazazi walishiriki nasi kwenye tukio hili, pichani ni mana mzazi wa mwanzilishi wa Smithmai, Maimuna Kiganza.

Tuesday, February 2, 2016

SMITHMAI: MUONEKANO MPYA WA VIATU NA MAVAZI!!!

Mwaka 2015, smithmai ilifanikiwa kutengeneza jumla ya design tano za viatu, ikiwa ni mara ya kwanza tangu Kampuni hii ianze kufanya kazi. Pichani ni design ya tatu kutengenezwa, inayojulikana kwa jina la Bflovelove.
Viatu vya smithmai ni viatu vinavyotengenezwa kwa ngozi asilia na kusanifiwa kwa malighafi za asili ya kitanzania. Pichani ni design ya kwanza ya viatu vya smithmai, vinavyojulikana kwa jina la Maimuna.
Ubunifu wa viatu, kwa kutumia shanga za aina tofauti tofauti katika kutengeneza maua ni miongoni mwa vitu ambavyo smithmai ilijaribu kuvifanya kwa mwaka 2015. Pichani ni Viatu vilivyotengenezwa kwa shanga, Viatu hivi vinajulikana kwa jina la cutemama. Ni design ya pili kutengenezwa na Kampuni ya Smithmai.

Mpaka Kufikia mwezi wa kumi mwaka jana, Smithmai ilifanikiwa kuwa na jumla ya design sita za viatu, ikiwa ni hatua ya kwanza ya uzalishaji na utengenezaji wa viatu vya Smithmai.  
Pichani ni design ya nne ya viatu, inayojulikana kama Maiken.

Friday, August 21, 2015

SMITHMAIDAY: TUWAPE KIPAUMBELE VIJANA WETU, KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU


Kampuni ya smithmai, ni kampuni mpya iliyosajiliwa mapema mwaka huu, inayojihusisha zaidi na vijana kwenye masuala ya kiuchumi, lengo likiwa kuchochea mabadiriko ya kiuchumi kwa vijana wa kitanzania na Afrika kwa ujumla. Kampuni hii ilianzishwa na kijana ambae pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu Kampala International University shahada ya sheria Maimuna Kiganza na kutambulishwa rasmi kwa jamii ta vijana, wazazi na makundi mengine ya kijamii  tarehe 27/05/2015.
Tarehe hiyo 27/05/2015 Kampuni ya smithmai pia ilizindua rasmi, siku maalum ya kuhamasisha vijana kujiajiri, pamoja na kuangalia namna ambavyo tunaweza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana wa kitanzania hususani katika kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi na kujiendeshea maisha yao wenyewe.
Mbali na kujihusiaha moja kwa moja na vijana katika masuala ya kiuchumi hususani katika ajira, uwekezaji na ushirikishwaji wa vijana, kampuni hii ya smithmai inajihusisha na utengenezaji wa viatu tofauti tofauti vyenye asili ya kiafrika zaidi zaidi,Tanzania ambavyo hutengenezwa kwa malighafi na rasilimali ambazo zinapatikana Tanzania ili kuwapa hamasa vijana wengine kuanza na vitu walivyonavyo ili kuondokana na utegemezi wa kiuchumi. 

Tuesday, June 2, 2015

TATIZO LA AJIRA NI LETU SOTE, TUSHIRIKIANE KULITATUA, INAWEZEKANA!!!

Wakati maandalizi ya kuiboresha blog hii yakiendelea, si vibaya tukaweka mambo mawili matatu huku tukisubiria kukamilika kwa blog hii mwezi huu. Swali la msingi ni unatumiaje simu yako ya mkononi, sasa hivi kuna vijana wengi ambao hawana ajira, ni tatizo kubwa kitaifa, tunahangaika sana kulitatua, wakati pengine tunaweza kulipatia ufumbuzi. Watu wengi tuna simu za mkononi, tena zenye kutuwezesha kupata huduma ya internet, iwapo tutajenga utamaduni mzuri wa matumizi mazuri ya simu za mkononi, pengine tunaweza kutatua tatizo la ajira. Moja kati ya vitu vinavyoifanya blog ya smithmai iwepo leo, ni matumizi mazuri ya Internet ya Mwanzilishi wa blog pamoja na Kampuni ya Smithmai, Maimuna Kasaim Kiganza. Yeye alikua na desturi ya kulike page za watu wenye kuleta tija na changamoto katika jamii, mmoja wapo Joyce Kiria. Na hapo ndipo alipopata fursa ya kukutana na Joyce Kiria. Ilikua baada ya kupokea Tangazo la kutafuta watu wakujitolea wiki 48 zilizopita kupitia mtandao wa facebook, ambalo lilikua na namba za simu na maelekezo ya kutuma maombi ya kujitolea kwa kutumia mtandao wa whatsapp. Alilichukulia tangazo lile kama fursa, na kulifanya hadi kuitwa kwenye usaili. Pichani ni mara baada ya kupita kwenye usaili, akiwa pamoja na watu wengine waliofanikiwa kupita usaili huo na Joyce Kiria mwenyewe (mkurugenzi mtendaji Wanawakelive).

Baada ya hapo, alipata nafasi ya kuwepo kwenye kikundi cha uchumi, lengo likiwa ni kumuwezesha mwanamke kuweza kujitegemea yeye binafsi kiuchumi, jambo hilo lilimfanya akatune na watu wengi ambao asingekutana nao sehemu nyengine yeyote zaidi ya kupitia platform ya wanawakelive, aliweza kupata mawazo mapya  kila kikundi kilipokuwa kinakutana, picha hii alipiga studio za bongo movies moja ya kipindi kinachoandaliwa chini ya management ya wanawakelive na ilikua siku kikundi cha uchumi kilipokutana, kujadiliana.
Hata hivyo, vikundi hivyo havikudumu kwa muda mrefu, kwasababu za kifedha. Watu wengi walipoona hakuna kipato chochote tunachoingiza zaidi ya kujadiliana mikakati na masuala ya kiuchumi, mmoja baada ya mwengine aliacha, hali iliyopelekea kufa kabisa kwa vikundi hivyo. Vilipokufa, Maimuna ilibidi amuombe Joyce Kiria nafasi ya kufanya kazi kwa kujitolea na ndipo hapo alipoitwa ofisini na kufanyiwa usaili wa pili,na mkuu wa vipindi kwa wakati huo Steven Lumati, baada ya hapo, akapata fursa ya kufanya kazi. Alikua hajui chochote, na ni mwanafunzi wa chuo tena ambae hana hata cheti cha taaluma, hivyo sehemu ya kwanza aliyoanza kufundishwa kazi ilikua kwenye website. Alianza anafundishwa na wafanyakazi ofisini mpaka akaja kujua, na huo ndio ulikua mwanzo na njia au ndoto za kuanzisha smithmai blog ulipozaliwa. 
Mbali ya kujifunza na kufanya kazi kwenye blog, pia alipata nafasi ya kufanya kazi sehemumbalimbali, na hii ni baada ya Joyce Kiria kuona uwezo aliokua nao lakini namna ambavyo alijitoa kufanya kazi, na hapo ndipo alipopata fursa ya kuambatana nae kwenye safari ya tabora mapema mwaka huu.
Wakati huu ambao, kuna tatizo kubwa la ajira ni vyema tukaanza kutumia vinavyojulikana, kutatua matatizo tuliyo nayo, matumizi mazuri ya simu na mitandao inaweza  kuwa njia mojawapo ya kutatua tatizo la ajira, iwapo tutaangalia suala hili katika jicho la tatu.