Wakati maandalizi ya kuiboresha blog hii yakiendelea, si vibaya tukaweka mambo mawili matatu huku tukisubiria kukamilika kwa blog hii mwezi huu. Swali la msingi ni unatumiaje simu yako ya mkononi, sasa hivi kuna vijana wengi ambao hawana ajira, ni tatizo kubwa kitaifa, tunahangaika sana kulitatua, wakati pengine tunaweza kulipatia ufumbuzi. Watu wengi tuna simu za mkononi, tena zenye kutuwezesha kupata huduma ya internet, iwapo tutajenga utamaduni mzuri wa matumizi mazuri ya simu za mkononi, pengine tunaweza kutatua tatizo la ajira. Moja kati ya vitu vinavyoifanya blog ya smithmai iwepo leo, ni matumizi mazuri ya Internet ya Mwanzilishi wa blog pamoja na Kampuni ya Smithmai, Maimuna Kasaim Kiganza. Yeye alikua na desturi ya kulike page za watu wenye kuleta tija na changamoto katika jamii, mmoja wapo Joyce Kiria. Na hapo ndipo alipopata fursa ya kukutana na Joyce Kiria. Ilikua baada ya kupokea Tangazo la kutafuta watu wakujitolea wiki 48 zilizopita kupitia mtandao wa facebook, ambalo lilikua na namba za simu na maelekezo ya kutuma maombi ya kujitolea kwa kutumia mtandao wa whatsapp. Alilichukulia tangazo lile kama fursa, na kulifanya hadi kuitwa kwenye usaili. Pichani ni mara baada ya kupita kwenye usaili, akiwa pamoja na watu wengine waliofanikiwa kupita usaili huo na Joyce Kiria mwenyewe (mkurugenzi mtendaji Wanawakelive).
Baada ya hapo, alipata nafasi ya kuwepo kwenye kikundi cha uchumi, lengo likiwa ni kumuwezesha mwanamke kuweza kujitegemea yeye binafsi kiuchumi, jambo hilo lilimfanya akatune na watu wengi ambao asingekutana nao sehemu nyengine yeyote zaidi ya kupitia platform ya wanawakelive, aliweza kupata mawazo mapya kila kikundi kilipokuwa kinakutana, picha hii alipiga studio za bongo movies moja ya kipindi kinachoandaliwa chini ya management ya wanawakelive na ilikua siku kikundi cha uchumi kilipokutana, kujadiliana.
Hata hivyo, vikundi hivyo havikudumu kwa muda mrefu, kwasababu za kifedha. Watu wengi walipoona hakuna kipato chochote tunachoingiza zaidi ya kujadiliana mikakati na masuala ya kiuchumi, mmoja baada ya mwengine aliacha, hali iliyopelekea kufa kabisa kwa vikundi hivyo. Vilipokufa, Maimuna ilibidi amuombe Joyce Kiria nafasi ya kufanya kazi kwa kujitolea na ndipo hapo alipoitwa ofisini na kufanyiwa usaili wa pili,na mkuu wa vipindi kwa wakati huo Steven Lumati, baada ya hapo, akapata fursa ya kufanya kazi. Alikua hajui chochote, na ni mwanafunzi wa chuo tena ambae hana hata cheti cha taaluma, hivyo sehemu ya kwanza aliyoanza kufundishwa kazi ilikua kwenye website. Alianza anafundishwa na wafanyakazi ofisini mpaka akaja kujua, na huo ndio ulikua mwanzo na njia au ndoto za kuanzisha smithmai blog ulipozaliwa.
Mbali ya kujifunza na kufanya kazi kwenye blog, pia alipata nafasi ya kufanya kazi sehemumbalimbali, na hii ni baada ya Joyce Kiria kuona uwezo aliokua nao lakini namna ambavyo alijitoa kufanya kazi, na hapo ndipo alipopata fursa ya kuambatana nae kwenye safari ya tabora mapema mwaka huu.
Wakati huu ambao, kuna tatizo kubwa la ajira ni vyema tukaanza kutumia vinavyojulikana, kutatua matatizo tuliyo nayo, matumizi mazuri ya simu na mitandao inaweza kuwa njia mojawapo ya kutatua tatizo la ajira, iwapo tutaangalia suala hili katika jicho la tatu.