Friday, August 21, 2015

SMITHMAIDAY: TUWAPE KIPAUMBELE VIJANA WETU, KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU


Kampuni ya smithmai, ni kampuni mpya iliyosajiliwa mapema mwaka huu, inayojihusisha zaidi na vijana kwenye masuala ya kiuchumi, lengo likiwa kuchochea mabadiriko ya kiuchumi kwa vijana wa kitanzania na Afrika kwa ujumla. Kampuni hii ilianzishwa na kijana ambae pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu Kampala International University shahada ya sheria Maimuna Kiganza na kutambulishwa rasmi kwa jamii ta vijana, wazazi na makundi mengine ya kijamii  tarehe 27/05/2015.
Tarehe hiyo 27/05/2015 Kampuni ya smithmai pia ilizindua rasmi, siku maalum ya kuhamasisha vijana kujiajiri, pamoja na kuangalia namna ambavyo tunaweza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana wa kitanzania hususani katika kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi na kujiendeshea maisha yao wenyewe.
Mbali na kujihusiaha moja kwa moja na vijana katika masuala ya kiuchumi hususani katika ajira, uwekezaji na ushirikishwaji wa vijana, kampuni hii ya smithmai inajihusisha na utengenezaji wa viatu tofauti tofauti vyenye asili ya kiafrika zaidi zaidi,Tanzania ambavyo hutengenezwa kwa malighafi na rasilimali ambazo zinapatikana Tanzania ili kuwapa hamasa vijana wengine kuanza na vitu walivyonavyo ili kuondokana na utegemezi wa kiuchumi.