Kumekua na wimbi kubwa sana la vijana wasiokuwana ajira, wengi wakiilalamikia serikali kutokana na tatizo hili la ajira, lakini wasichokijua ni kwamba kazi yeyote ya halali inafaida, si lazima mpaka uwe umeajiriwa serikalini au sekta binafsi ndiyo uweze kuendesha maisha yako, hata biashara na ujasiriamali unaweza kukufanya kuendesha maisha yako vizuri kuliko vile ambavyo ungeajiriwa na mtu.
Ukigusa tu suala la kujiajiri, wapo watakaokwambia unaanzaje kujiajiri wakati mtaji ni changamoto, napenda nitumie fursa hii kukwambia anza na ulicho nacho katika kutekeleza mipango yako mbalimbali ya kimaendeleo, usisubiri kuwezeshwa, anza wale wa kukuwezesha wawe wa ziada lakini si tegemezi kwako. Kwa mfano wewe huna mtaji ila unauwezo wa kusuka watu nywele, anza kwa kuwasuka watu nywele upate mtaji wa kuanzisha biashara yako, au unanguvu huna kazi au mtaji wa kufanya miradi yako uliyoipanga, anza kwa kutumia hizo nguvu zako kutafuta pesa itakayokuwezesha kupata mtaji, kama ni kumsaidia mtu kupika mama ntilie, kufyatua matofali, kuuza dagaa sokoni kama huyo mdada pichani we anza tu ili mradi ujue kabisa lengo la kufanya biashara au kazi au chochote utakachoanza nacho ni kupata mtaji utakaokuwezesha kujiajiri au kufanya mambo yako mengine.
Usiogope kufanya au kujishughulisha na shughuli yeyote, hata ikiwa kujitwisha beseni la mboga mboga, na kutembeza wewe fanya ili mradi kichwani kwako uwe na target kwamba leo nafanya biashara hii kwa kutembeza, lengo langu ni nipate mtaji wa kufanya kitu flani, wakati nikiwa naendelea kutafuta mtaji nitaboresha biashara yangu hii ili iendane na hadhi ninayoitaka, kama nilikua natembea kwa miguu, nitanunua baiskeli ili inirahisishie kazi na pia kuwafikia wateja wengi zaidi, kitakachofuata labda niwe na kituo changu cha usambazaji na niwe na watu wawili, watatu wa kunisaidia wakati huo nikiwa katika mchakato wa kuanzisha biashara yangu n.k
Lakini si vyema kuwahusisha watoto katika shughuli hizi na zinginezo za kibiashara na maendeleo kwa maana ya kujiajiri kwasababu utakuwa unamnyima mtoto fursa yake ya kuwa mtoto na kufanya mambo ya umri wake kama watoto wengine wa umri kama wake wanavyofanya ikiwa ni pamoja na elimu. Inawezekana kupiga hatua ya kimaendeleo, kujiajiri au hata kutimiza ndoto zako, anza leo tena anza na ulicho nacho. Hata katika imani zetu za dini (kwa wanao amini uwepo wa Mungu kama mimi) Mungu alimruhusu Mussa (Moses) kufanya makubwa kwa kuanza na alicho nacho mkononi ambacho ni fimbo, kwahiyo hata wewe unaweza kufanya makubwa iwapo utatathubutu kuanza na ulichonacho.
No comments:
Post a Comment