Friday, August 21, 2015

SMITHMAIDAY: TUWAPE KIPAUMBELE VIJANA WETU, KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU


Kampuni ya smithmai, ni kampuni mpya iliyosajiliwa mapema mwaka huu, inayojihusisha zaidi na vijana kwenye masuala ya kiuchumi, lengo likiwa kuchochea mabadiriko ya kiuchumi kwa vijana wa kitanzania na Afrika kwa ujumla. Kampuni hii ilianzishwa na kijana ambae pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu Kampala International University shahada ya sheria Maimuna Kiganza na kutambulishwa rasmi kwa jamii ta vijana, wazazi na makundi mengine ya kijamii  tarehe 27/05/2015.
Tarehe hiyo 27/05/2015 Kampuni ya smithmai pia ilizindua rasmi, siku maalum ya kuhamasisha vijana kujiajiri, pamoja na kuangalia namna ambavyo tunaweza kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana wa kitanzania hususani katika kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi na kujiendeshea maisha yao wenyewe.
Mbali na kujihusiaha moja kwa moja na vijana katika masuala ya kiuchumi hususani katika ajira, uwekezaji na ushirikishwaji wa vijana, kampuni hii ya smithmai inajihusisha na utengenezaji wa viatu tofauti tofauti vyenye asili ya kiafrika zaidi zaidi,Tanzania ambavyo hutengenezwa kwa malighafi na rasilimali ambazo zinapatikana Tanzania ili kuwapa hamasa vijana wengine kuanza na vitu walivyonavyo ili kuondokana na utegemezi wa kiuchumi. 

Tuesday, June 2, 2015

TATIZO LA AJIRA NI LETU SOTE, TUSHIRIKIANE KULITATUA, INAWEZEKANA!!!

Wakati maandalizi ya kuiboresha blog hii yakiendelea, si vibaya tukaweka mambo mawili matatu huku tukisubiria kukamilika kwa blog hii mwezi huu. Swali la msingi ni unatumiaje simu yako ya mkononi, sasa hivi kuna vijana wengi ambao hawana ajira, ni tatizo kubwa kitaifa, tunahangaika sana kulitatua, wakati pengine tunaweza kulipatia ufumbuzi. Watu wengi tuna simu za mkononi, tena zenye kutuwezesha kupata huduma ya internet, iwapo tutajenga utamaduni mzuri wa matumizi mazuri ya simu za mkononi, pengine tunaweza kutatua tatizo la ajira. Moja kati ya vitu vinavyoifanya blog ya smithmai iwepo leo, ni matumizi mazuri ya Internet ya Mwanzilishi wa blog pamoja na Kampuni ya Smithmai, Maimuna Kasaim Kiganza. Yeye alikua na desturi ya kulike page za watu wenye kuleta tija na changamoto katika jamii, mmoja wapo Joyce Kiria. Na hapo ndipo alipopata fursa ya kukutana na Joyce Kiria. Ilikua baada ya kupokea Tangazo la kutafuta watu wakujitolea wiki 48 zilizopita kupitia mtandao wa facebook, ambalo lilikua na namba za simu na maelekezo ya kutuma maombi ya kujitolea kwa kutumia mtandao wa whatsapp. Alilichukulia tangazo lile kama fursa, na kulifanya hadi kuitwa kwenye usaili. Pichani ni mara baada ya kupita kwenye usaili, akiwa pamoja na watu wengine waliofanikiwa kupita usaili huo na Joyce Kiria mwenyewe (mkurugenzi mtendaji Wanawakelive).

Baada ya hapo, alipata nafasi ya kuwepo kwenye kikundi cha uchumi, lengo likiwa ni kumuwezesha mwanamke kuweza kujitegemea yeye binafsi kiuchumi, jambo hilo lilimfanya akatune na watu wengi ambao asingekutana nao sehemu nyengine yeyote zaidi ya kupitia platform ya wanawakelive, aliweza kupata mawazo mapya  kila kikundi kilipokuwa kinakutana, picha hii alipiga studio za bongo movies moja ya kipindi kinachoandaliwa chini ya management ya wanawakelive na ilikua siku kikundi cha uchumi kilipokutana, kujadiliana.
Hata hivyo, vikundi hivyo havikudumu kwa muda mrefu, kwasababu za kifedha. Watu wengi walipoona hakuna kipato chochote tunachoingiza zaidi ya kujadiliana mikakati na masuala ya kiuchumi, mmoja baada ya mwengine aliacha, hali iliyopelekea kufa kabisa kwa vikundi hivyo. Vilipokufa, Maimuna ilibidi amuombe Joyce Kiria nafasi ya kufanya kazi kwa kujitolea na ndipo hapo alipoitwa ofisini na kufanyiwa usaili wa pili,na mkuu wa vipindi kwa wakati huo Steven Lumati, baada ya hapo, akapata fursa ya kufanya kazi. Alikua hajui chochote, na ni mwanafunzi wa chuo tena ambae hana hata cheti cha taaluma, hivyo sehemu ya kwanza aliyoanza kufundishwa kazi ilikua kwenye website. Alianza anafundishwa na wafanyakazi ofisini mpaka akaja kujua, na huo ndio ulikua mwanzo na njia au ndoto za kuanzisha smithmai blog ulipozaliwa. 
Mbali ya kujifunza na kufanya kazi kwenye blog, pia alipata nafasi ya kufanya kazi sehemumbalimbali, na hii ni baada ya Joyce Kiria kuona uwezo aliokua nao lakini namna ambavyo alijitoa kufanya kazi, na hapo ndipo alipopata fursa ya kuambatana nae kwenye safari ya tabora mapema mwaka huu.
Wakati huu ambao, kuna tatizo kubwa la ajira ni vyema tukaanza kutumia vinavyojulikana, kutatua matatizo tuliyo nayo, matumizi mazuri ya simu na mitandao inaweza  kuwa njia mojawapo ya kutatua tatizo la ajira, iwapo tutaangalia suala hili katika jicho la tatu.

Tuesday, April 28, 2015

Mradi wa mkaa Endelevu wilayani Kilosa.

Kama huo mchoro uunavyoonesha hapo, kitu chochote katika maisha, jambo lolote ambalo uunaliona wewe, linaanza na kufikiria wazo, ukishapata wazo na ukawa na utayari na nia ya kulifanya, hapo ndipo njia na milango hufunguka. Tatizo kubwa linalotusumbua watanzania ni uvivu wetu wa kufikiria hali inayopelekea wengi wetu kutokua na malengo au mipango mikakati ya maisha yetu. Kwenye baadhi ya maeneo, ambayo wamebahatika kuwa na viongozi bora, angalau viongozi wale wameweza kuwafunua macho wananchi wao, na kuthubutu pamoja kufanya kitu cha utofauti, mojawapo wa eneo hilo, ni wilaya ya Kilosa, kupitia mradi wa mkaa endelevu. 
Mradi wa mkaa endelevu hadi kufikia mwezi wa nane mwaka jana, ulikua umetimiza miaka miwili kwa maana hiyo mradi wa mkaa endelevu, ulianzishwa mwaka 2013 huko wilayani kilosa mkoa wa morogoro.  Watunga, watekelezaji sera na miongozo kwa kushirikiana na wananchi waliona tatizo lilokuwepo ambalo lilitokana na kupigwa marufuku kwa ukataji wa mkaa hali iliyopelekea watu wengu kufanya shughuli hio kwa magendo, njia za panya na ambayo ilikua haina maslahi makubwa kwa pande zote, wafanyaji wa shughuli hiyo na, watu wa eneo hilo na hata upande wa serikali. Waliona kuwa ukataji na uvunaji wa mkaa ni sehemu au chanzo kikubwa cha kipato cha wananchi wa enei lao hivyo waliamua kuja na njia ambayo ingekua suluhusho la kudumu kwa pande zote, na pia kutokuharibu mazingira kwa kuja na mradi wa mkaa endelevu.

Wakaja na njia ya kutenga maeneo ya misitu maalum kwa kwa ajili ya uvunaji wa mkaa endelevu yalipo chini ya sheria na taratibu halali. Wakaunda na  taratibu za kuwepo kwa utoaji vibali, ambavyo vinalipiwa kwa mujibu na taratibu za kisheria, pia wakaweka na ushuru wa mkaa ambao wavunaji wanapaswa kulipia kwa maendeleo ya eneo lao  lakini pia kuweka usimamizi shirikishi wa misitu ili kudhibiti shughuli zozote za uvunaji wa mkaa ambazo zinaenda kinyume na taratibu. Kitendo hicho kimewezesha halmashauri yao kupata mapato ambayo yamechangia kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa zahanati la eneo hilo, nyumba ya mganga (daktari) wa zahanati, madawati ya wanafunzi eneo hilo, nyumba za walimu, na kuweka maazimio ya kununua pikipiki itakayosimamia shughuli za maliasili.
Fedha zilizotoka kwenye mradi huu wa mkaa endelevu, zimiiwezesha kilosa kufanya mambo mengi ya kimaendeleo kuliko fedha zilitoka serikalini. Pia mradi huu umewezesha mahusiano mazuri baina ya wananchi na viongozi wao, zaidi ya hilo umetoa motisha kwa wananchi kushiriki katika kusimamia misitu na hivyo kupunguza uharigu. Kubwa kabisa ambalo mradi huu umefanya ni, kuongeza ushindani kati ya mkaa unaotokana na kinyume cha sheria na mkaa ambao unatokana na mradi huu, kwani mkao unaotokana na mradi huu una ubora zaidi kuliko mkaa unaotengenezwa kimagendo, hivyo kuwafanya wavunaji wengi kubaki njia kuu, kwasababu michepuko haiwaingizii faida.
Maeneo yanapobaki bila kusimamiwa yanakua ni hifadhi ya waalifu, na watu wanapobaki bila kazi za kufanya kunawafanya waingie kwenye uhalifu. Tanzania ni nchi ambayo imejaaliwa kuwa na eneo kubwa la ardhi, na baadhi ya maeneo hayatumiki, Tanzania pia imejaaliwa kuwa na idadi kubwa ya nguvu kazi ambapo asilimia 60ya watu wake ni vijana. Iwapo kama Tanzania, na sisi watanzania wenyewe tutaangalia ardhi na maeneo tuliyo nayo, tutaangalia nguvu kazi tuliyonayo na mahitaji yao, ndami ya miaka 30 ijayo tutakuwa katika ramani nyengine kabisa duniani, ukiachilia mbali utalii, na vivutio vingine vilivyopo, ukiachilia mbali madini na rasilimali zingine tulizo nazo. Tanzania ni tajiri mno, ila tatizo ni, sisi watanzania ni wavivu wa kufikiri.

#My body in&out: Fahamu kuhusu tatizo la Ovarian Cyst(vijivimbe kwenye mifuko yw mayai ya uzazi wa mwanamke)

Ovarian cyst ni tatizo la kuwepo kwa vijiuvimbe vidogo vidogo kwenye mayai ya uzazi ya mwanamke, tatizo hili linasababishwa na kuzidi au kupungua kwa homoni mbalimbali katika mwili wa mwanamke na dalili zake n;
a) maumivu makali chini ya kitovu,
b) kuvuja damu ndani kwa ndani
C) kupata tatizo la tumbo kujaa gesi ambalo linasababisha kutokumengenywa kwa chakula  vizuri na hivyo kusababisha maumivu makubwa wakati wa haja kubwa. 
d) kushindwa kumaliza mkojo, namaanisha kwenda haja ndogo (kukojoa) mara kwa mara, ili hali mwanamama au binti huyo hana tatizo la kisukari au yutiyai.
e) Kupata maumivu makali kabla ya period, baada au wakati wa period.
f) kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
g)  vagina bleeding au kwa lugha nyengine kupata damu kama ya hedhi katika vipindi ambavyo havitarajawi, nikimaanisha anaweza kumaliza siku zake leo, baada ya siku tatu au wiki akarudia tena.
Pia dalili nyengine ni kutokuwa na mzunguko wa hedhi unaoleweka (fixed period) na ya mwisho katika uelewa wangu ni kupata dalili za ujauzito wakati binti au mwanamke huyo si mjamzito.

Pindi vijiuvimbe hivi vikikua sana, na kila kimoja kujiongeza (kujimultiply) vinaathiri viungo vingine vya uzazi na kusababisha kuvimba kwa mirija ya uzazi na hivyo kupelekea utasa.

 Endometriosis ni moja ya tatizo linalotokan na a kuwepo kwa vijiumbe hivi kwenye mifuko ya uzazi wa mwanamke.

Sunday, April 12, 2015

VITU MUHIMU VYA KUFUNGUA MAFANIKIO, (THE MOST CRUCIAL KEY TO SUCCESS)

Kuna vitu ambavyo ni kama ufunguo wa mafanikio. Vitu hivyo ni

a) Elimu
b)Uadilifu
c)Tabia za mtu binafsi
d)Akili
e) Ubunifu

There are things that act as keys towards success, these are
a) Education
b) Integrity
c) Personal habits
d) Intelligence
e) Initiatives

Ili mtu aweze kufanikiwa katika maisha ni lazima awe na Elimu kuhusiana na kile kitu anachotaka kukifanya, kuwa na elimu kutamsaidia kupambanua masuala mbalimbali anayokumbana nayo lakini pia kuleta tija katika kitu anachokifanya.


 For a person to be successful in life, first he must acquire education, concerning particular thing that he ought to do, having education will help that person in ackowleding and solving different challenges and thus enhence productivity on that particular matter.
Pia mtu anapaswa kuwa na uadilifu katika kile kitu anachokifanya,  uadilifu ni kile kitendo cha kuchagua mawazo na matendo yako yaongozwe na vipaumbele vyako kuliko kile kipato utakachokipata. Unapo ishi kuendena na vipaumbele vyako katika maisha yako, unajipa nafasi ya kujitathimini na kujipima kiwango gani umefikia kwa wakati husika, wapi pana mapungufu na jinsi gani ya kukabiliana nayo, yapi umetimiza kwa wakati na yapi hayajafanikiwa na jinsi ya kujiboresha.
However, a person needs to have integrity towards whatever thing he or she does, Integrity is choosing your thought and actions based on values rather than personal gain. Living and doing things based on your values paves a way to self evaluation and determination  of the goals you had set before, that way you will be able to discover the strength, potential and weakness you had achive and how to improve.
Kingine ni, tabia za mtu binafsi, kama vile vitu anavyopendelea kuvifanya na namna ambavyo anavyoishi na watu wanaomzunguka wakiwemo anaofanya nao kazi. Mara nyingi  vile unavyoishi na watu inaweza kuchochea au kuporomosha maendeleo au hata mafanikio yako. Ukiwa ni mtu wa kutokuthamini mawazo na michango ya wengine, au zile kazi zao, watu wengi watashindwa kufanya kazi na wewe na hata utendaji kazi wa watakao kua wanafanya utakuwa hafifu, na hivyo kuchangia katika kuporomosha mafanikio yako, lakini ukiwa mtu wa kuthamini kazi na michango ya wengine, itachochea katika uwajibikaji na uzalishaji.

Moreover personal habits, contribute much to a person achievements, the things one does for oneself, the way he or she relate with others, the co workers or employees inclusive. usually how one relate with other may prosper or act as hindrance to a persons towards sucess. If you are a kind of person that doesn"t appreciate or value other peoples opinion, no body will be confortable working with you, or work for you and even when they do, they might not work with such high passion and willinges of adding a value and progress into such work place, contrary to if you were a different person, and most probably a person who appreciate and value other peoples work, suggestion, and contribution.
Pia kuwa na akili au upeo wa kuona mbali zaidi, na kuangalia kila kitu katika eneo linalokuzunguka kama fursa ya wewe kujiongezea kipato au kupata mafanikio. Tatizo lolote kwenye jamii, ukiweza kulitatua basi linakuwa fursa ya kiuchumi kwako. Kitu hiko hiko mtu mwengine anachokifanya, ukiwa na akili ya ziada kuongeza ubunifu na utofauti kati yako naye, tayari utakua umetengeneza fursa, masoko au hata kipato. Kifanye kitu chako, kazi yako, biashara yako, iwe na utofauti na wengine ili impe mtu sababu kwanini afanye biashara na wewe, asifanye na wengine, kwanini anunue bidhaa yako wewe asinunue ya mwengine, hiyo itakuweka katika nafasi nzuri ya kufanikiwa.
Success also entails the intelligence or thinking capacity that one has,  the ability to look beyond, and looking at opportunities around the area one belongs. Any problem that your community faces, if you find solution to that problem, then that problem changes and become a source of economy to you. The same thing that some one else is doing,if you find  you can find that thinking ability to formulate or do thar particular thing in a very unique way, that will let someone find a reason of doing business with you and not with other, why that person should take your service and not others, then it will put you in a great position to succeed.


Cha mwisho ni kutengeneza kitu (ubunifu). Kwa mfano, unapenda kuwa muimbaji, buni aina ya muziki unaotaka kuimba ambayo itaendana na uhalisia wako na ambayo itakupa furaha, kitendo tu cha kufanya kile kitu unapata furaha. Kukifurahia kitu unachokifanya kitakuwezesha wewe kutengeneza (kubuni) vitu tofauti tofauti katika kitu unachokifanya ambacho kitapelekea kuongeza ubora wa kazi yako, na pia kuongeza kipato, hivyo hii pia itakusaidia katika kufikia mafanikio yako. 
And the last, is initiatives. For instance, you love to be a singer, initiate the kind of music that you will love to sing, the kind of music that will meet your personal desires, and that will bring happiness to you. When what you love to do, attracts happiness towards you, youwill find the desire to initiate different things that will add a value to what you are doing and which will increase your income possession, this will lead you towards your personal success.


Friday, April 10, 2015

SABABU YA KUFANYA KITU UNACHOKIPENDA

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kufanya kitu kwasababu unakipenda, au kwasababu unapendelea kukifanya na kukifanya kwasababu kinakupa fedha.Nimekua nikijiuliza maswali mengi siku hizi za karibuni, hivi kitu gani nikikifanya kina nipa furaha na uhuru ule wa  ndani yangu, na kila ninapojiuliza ndipo nakaribia kujua kitu gani hasa napendelea. Ukijaribu kuangalia, ndani yako utagundua kuwa kuna vitu huvipendi, na kuna vitu unavipenda, na hii ipo katika maeneo yote ya maisha. Ili uweze kuishi kwa amani, ni lazima ujue kitu gani ukikafanya kinakupa furaha, mtu gani ukikaa nae chini ukazungumza nae, anakufanya upunguze labda uchovu, kukata tamaa n.k. Kila mtu ana upekee wake na namna ambavyo anaweza kugusa maisha ya wengine au kuwafanya watambue ndoto zao, malengo yao, watu ambao wanataka kuwa nao kwa maisha yao yote n.k, unatakiwa ujue hiko kitu au huyo mtu ili uweze kuwa na ndoto za kutimiza, na sababu ya kuamka asubuhi kwenda kufanya kazi.

Ukisha jua huyo mtu ambae anaweza kukufanya utambue nini hasa kinakupa ule uhuru wa ndani yako na ile furaha ya kudumu, jaribu kutafuta kazi yako katika maisha haya, tatizo linalowafanya waafrika na watanzania wengi kutokufika mbali kimaendeleo ni kutokujua kitu gani hasa ni kazi zao hasa ambazo wanapaswa kuzifanya. Hii inatokana na mifumo ya elimu tuliyonayo lakini pia mawazo ambayo tumejiwekea, ya kusoma ili tuajiriwe badala yakusoma ili tupate ile furaha ya kufanya kitu tunachopendelea kukifanya. Sababu ya watuwengi wa njee kuendelea ni kuishi kwenye yale mambo ambayo kwanza wanayaweza lakini pili yanayowapa furaha. Mfano ni Alicia Keys
Yeye alizaliwa tarehe 26 January mwaka 1981, na kuanza kujifunza muziki kwa kuchukua somo la kwaya kama soko kuu. Tangu ahitimu alipokua na umri wa miaka 7 mpaka sasa amekua akifanya muziki. Ni mwanamuziki aliyedumu kwa miaka mingi kwenye muziki bila ya kuwa na skendo za aina yeyote ile. Ni mwanamuziki mwenye mafanikio sana katika muziki lakini pia kujizolea tuzo nyingi kama za Bilbord, MTV music award, America music award n.k
Kitu chochote kile au ujuzi wowote ule ambao mtu anaamua kuuchukua, lengo kuu ni kupata uhakika wa kuishi maisha vizuri na kupata nafasi ya kuihudumia familia yake vyema. Hata sababu ya vijana wengi kukimbilia kwenye siasa kwa wingi kuliko sehemu nyengine ni kwasababu kwenye siasa kuna uhakika mkubwa au ulinzi mzuri wa kupata maisha bora kwa mtu binafsi na familia yake. Lakini kitu ambacho wengi tunakisahau ni  kitu chochote ambacho utakifanya goal yako, kwa maana ya ndoto unayoifanyia kazi na kuiwekea ukomo kwamba, kutoka muda flani hadi muda flani nataka niwe nimefanikisha kitu flani, basi unaweza kupata ulinzi, uhakika au security ambayo unaitafuta kwenye mambo mengine yakiwemo kama siasa.

Saturday, March 28, 2015

BINTI CHINI YA MIAKA 18, BADO NI MTOTO.


Miaka inaenda sana, na kwa sasa tupo katikati mwa karne ya 21, karne ambayo inaongozwa na mapinduzi ya taarifa au habari, kwa lugha ya kingereza inajulikana kama information age. Sasa hivi kufuatia kukua kwa teknolojia ya mawasilano, taarifa na habari nyingi husambaa kwa kasi zaidi, na kwa muda mfupi kuliko vile ilivyokua mwanzo, kwa maana hiyo maisha sasa yamebadirika sana, hivyo sisi Watanzania tunapaswa kukubali na kuendana na hali halisi ya maisha iliyopo kwa sasa. Hatuna budi kuachana na mila kandamizi zenye kuleta maumivu kwa wanawake na watoto ili tuweze kupambana kwenye karne hii ya 21 ya utandawazi kwa ujumla, kwasababu sasa dunia ni kama kijiji.Fursa zimeongezeka sana, lakini pia maovu mengi ni rahisi kuonekana Dunia nzima kwa muda mfupi sana, kuliko ilivyokua zamani.

Hakuna Taifa lililoendelea Duniani, ambalo Wanawake wake hawana Elimu,au hawajaenda shule. Hakuna taifa lililoendelea Duniani ambalo wanawake
wake waliozeshwa mapema na kukosa fursa ya kusoma, kufanya kazi na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi yao, kuwaozesha mabinti mapema ni kukuza ukandamizaji wa wanawake na kuongeza Idadi ya Wanawake walio tegemezi nchini.

Ifike wakati, mtoto apate haki zake stahiki pasipo kuidai au kushurtisha wazazi na serikali watambue mahitaji yao kama inavyoonekana hapo kwenye picha, hao ni wasichana wa shule za sekondari huko shinyanga wakilia sana na kupinga wao kuolewa mapema huku wakisema "Hatutaki kuolewa, Tunataka kusoma". Kwa dunia hii ya sasa, yenye mapinduzi makubwa ya taarifa na habari, unapomnyima msichana fursa ya kusoma kwa kumuozesha mapema unamfanya awe tegemezi kwa wazazi au mwanaume atakae enda kuishi nae, ukijumuisha hali ngumu ya maisha iliyopo kwa sasa, kila kitu kina gharama kubwa, anapomtegemea mwanaume kwa kila kitu inaongeza unyanyasaji na matukio ya kikatili wanaofanyiwa wanawake kutokana hawawezi kuendesha maisha yao bila kuwategemea wanaume wao.
Watoto wote duniani huzaliwa sawa, na hufuata hatua zote za ukuaji kulingana na umri walionao na makuzi au mazingira waliyolelewa, hivyo kumuozesha au kushiriki kimapenzi na binti aliye na umri chini ya miaka 18, ni kumdhalisha na kumfanyia ukatili wa kingono, kwasababu maumbo yao ndiyo yamekua lakini upeo wao wa kufikiria na kuchanganua bado haujakua kiasi cha kufanya maamuzo sahihi kuhusiana na afya za miili yao. Hivyo jmii, wazazi na serikali tunajukumu la kuwalinda mabinti chini ya miaka 18, kuwaelimisha kuhusu afya zao na mahusiano ya kimapenzi chini ya umri wa miaka 18, na changamoto zake.



Friday, March 27, 2015

KURA YANGU NI CHACHU YA MAENDELEO!!!

Hii picha nilipiga mwezi wa 12 mwaka jana, mara baada ya kutekeleza Haki na wajibu

Wangu, mimi mtanzania kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwezi wa 12 mwaka jana. Watanzania wengi tumekua na tabia ya kulaumu tu kuwa viongozi waliopo madarakani hawatimizi wanayopaswa kuyafanya kama viongozi na wawakilishi wetu, lakini ukija kuangalia kwa kiasi kikubwa Watanzania tulio wengi hatushiriki katika kuwachagua viongozi ambao tunawalalamikia, huwenda kwa kutokujua au tu kupuuzia na matokeo yake  masuala mbalimbali ya kimaendeleo yamekua yakichelewa wakati mwengine kutokufanyika kabisa, na wakati mwengine madhara makubwa kutokea kwenye jamii yetu kutokana ba viongozi na watendaji wazembe waliopo.

Kura yangu inanafasi kubwa sana ya kubadilisha mambo mbalimbali yanayoizinguka jamii yangu, iwapo tutajijengea utamaduni wa kupiga kura, kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyo sasa basi matatizo mengi yaliyopo katika jamii kwa sasa yatatatulika kwasababu njia pekee ya kumuwajibisha mtu asiyetenda au kutimiza wajibu wake kiurahisi ni kwa kupitia sanduku la kura.
Sanduku hili litakuwa muamuzi wa kiutendaji wa watu tunaowapa dhamana ya kuwa wawakilishi wetu sehemu mbalimbali, na kwa namna hiyo viongozi wengi wataanza kuwajibika kwasababu sanduku la kura litakuwa linahusika kila baada ya awamu kuisha, kupima masuala yao ya kiutendaji, ikiwa ni pamoja na kwenda kinyume na vitu walivyoahidi au ambavyo walishindwa kutekeleza kabisa.
Wakati umefika sasa kwa wanawake kujua thamani ya kura zetu badala ya kuwapigia watu kura kwasababu ya kitu cha siku moja ambacho kitakuacha muda mrefu kuumia kutokana na utendaji wao mbovu, chagua mtu si kwasababu anakupa kitu, chagua mtu kwasababu anauwezo na vigezo vya kutimiza malengo ya sehemu ulipo, nchi uliyopo na mwenye uwezo wa kutatua changamoto tulizonazo.
Kuelekea uchaguzi mkuu, ifanye kura yako/yangu iwe chachu ya maendeleo yetu.


Wednesday, March 25, 2015

KAZI YEYOTE HALALI INAFAIDA

 Kumekua na wimbi kubwa sana la vijana wasiokuwana ajira, wengi wakiilalamikia serikali kutokana na tatizo hili la ajira, lakini wasichokijua ni kwamba kazi yeyote ya halali inafaida, si lazima mpaka uwe umeajiriwa serikalini au sekta binafsi ndiyo uweze kuendesha maisha yako, hata biashara na ujasiriamali unaweza kukufanya kuendesha maisha yako vizuri kuliko vile ambavyo ungeajiriwa na mtu.
Ukigusa tu suala la kujiajiri, wapo watakaokwambia unaanzaje kujiajiri wakati mtaji ni changamoto, napenda nitumie fursa hii kukwambia anza na ulicho nacho katika kutekeleza mipango yako mbalimbali ya kimaendeleo, usisubiri kuwezeshwa, anza wale wa kukuwezesha wawe wa ziada lakini si tegemezi kwako. Kwa mfano wewe huna mtaji ila unauwezo wa kusuka watu nywele, anza kwa kuwasuka watu nywele upate mtaji wa kuanzisha biashara yako, au unanguvu huna kazi au mtaji wa kufanya miradi yako uliyoipanga, anza kwa kutumia hizo nguvu zako kutafuta pesa itakayokuwezesha kupata mtaji, kama ni kumsaidia mtu kupika mama ntilie, kufyatua matofali, kuuza dagaa sokoni kama huyo mdada pichani we anza tu ili mradi ujue kabisa lengo la kufanya biashara au kazi au chochote utakachoanza nacho ni kupata mtaji utakaokuwezesha kujiajiri au kufanya mambo yako mengine.
Usiogope kufanya au kujishughulisha na shughuli yeyote, hata ikiwa kujitwisha beseni la mboga mboga, na kutembeza wewe fanya ili mradi kichwani kwako uwe na target kwamba leo nafanya biashara hii kwa kutembeza, lengo langu ni nipate mtaji wa kufanya kitu flani, wakati nikiwa naendelea kutafuta  mtaji nitaboresha biashara yangu hii ili iendane na hadhi ninayoitaka, kama nilikua natembea kwa miguu, nitanunua baiskeli ili inirahisishie kazi na pia kuwafikia wateja wengi zaidi, kitakachofuata labda niwe na kituo changu cha usambazaji na niwe na watu wawili, watatu wa kunisaidia wakati huo nikiwa katika mchakato wa kuanzisha biashara yangu n.k


Lakini si vyema kuwahusisha watoto katika shughuli hizi na zinginezo za kibiashara na maendeleo kwa maana ya kujiajiri kwasababu utakuwa unamnyima mtoto fursa yake ya kuwa mtoto na kufanya mambo ya umri wake kama watoto wengine wa umri kama wake wanavyofanya ikiwa ni pamoja na elimu. Inawezekana kupiga hatua ya kimaendeleo, kujiajiri au hata kutimiza ndoto zako, anza leo tena anza na ulicho nacho. Hata katika imani zetu za  dini (kwa wanao amini uwepo wa Mungu kama mimi) Mungu alimruhusu Mussa (Moses) kufanya makubwa kwa kuanza na alicho nacho mkononi ambacho ni fimbo, kwahiyo hata wewe unaweza kufanya makubwa iwapo utatathubutu kuanza na ulichonacho.

"Magonjwa ya Akili ni magonjwa kama magonjwa mengine" Daktari Ruta(kitengo cha magonjwa ya akili hospitali ya taifa muhimbili)

Tarehe 08/02/2015 nilibahatika kuongozana na mdau na mwanaharakati mkubwa wa haki za wanawake na watoto, Joyce kiria kufuatilia tukio la mwanamke mmoja huko tabora ambae alifahamika kwa jina moja Bi Zuhura, kuwaua watoto wake wawili na kisha kuwafukia kwenye nyumba aliyokua anaishi. Safari yetu ilikua na changamoto nyingi ambapo gari ilituharibikia na hivyo tulilazimika kuchukua bus, ambayo ilitupa changamoto ya kusahau vifaa, kuchelewa n.k lakini tulifanikisha.
Kesho yake asubuhi tulianza safari ya kuelekea kwenye tukio, na kweli tulifika kwa msaada wa kapipi (mwandishi wa habari wa channel ten) ambaye alifuatilia kwa karibu tukio hili tangu siku ya kwanza lilivyotokea, na kwa habari tulizozipata hapo, kutoka kwa wahusika, yaani ndugu na majirani, pia mashuhuda wa tukio hilo kwa maana ya watu wa mwanzo walioona na pia kufuatilia tukio hilo ambae mmoja wapo, ni huyo mwandishi wa habari wa channel ten kuwa muhusika alikua na matatizo ya akili, na kwa maelezo yaliyotoka kwa babu yake Bi  Zuhura, mzee Shabani Ramadhani Kanene, faili la ugonjwa huo lilifunguliwa hospitali kitete Tabora na kwamba Bi Zuhura alipata ugonjwa huo mara baada ya kumzaa mtoto wake wa pili ambaye kwa sasa ni marehemu, ambapo inadaiwa aliuwawa na mama yake huyo baada  ya kumzidishia dawa alipokua anaumwa.
Mara baada ya kutoka eneo tukio hilo la kinyama lilipofanyika, safari ya kumtafuta baba mzazi wa marehemu ambae pia alikua mume halali wa Bi Zuhura, Bwana Mrisho ilianza, tulipata ushirikiano mzuri wa watu mbalimbali kutufikisha tulipopahitaji na muhusika (mume wa Bi Zuhura) alitueleza mambo mengi, likiwemo la kumuomba mana mzazi wa Bi Zuhura awachukue hao watoto kutokana na hali yake kiafya kutokua nzuri lakini Bi Zuhura na babu yake walikataa, alieleza.
Tuliporudi, tulimtafuta mtaalam wa magonjwa ya akili ambae ni daktari Ruta kutoka hospitali ya Taifa muhimbili, ambae alitueleza kuwa "magonjwa ya akili ni kama magonjwa mengine, na yanatibika iwapo yatawahi kupatiwa tiba ya uhakika, kwa kiwango kinachostahili na kwa wakati" alieleza zaidi kuwa wapo ambao wanapona kabisa na kurudi kwenye hali zao za kawaida, wapo ambao watatumia dawa maisha yao yote lakini wataweza kuendelea na shughuli zao za kila siku. Alisema magonjwa ya akili yapo ya aina makubwa na madogo,  na alisema tafsiri ya magonjwa ya akili ni magonjwa yanayoathiri mfumo mkubwa wa fahamu na kutibua visafirisha habari kwenye ubongo. 
Nilijifunza mengi na kwa hayo machache ni matumaini yangu na wewe umejifunza kitu, cha muhimu cha kuzingatia ni kwamba magonjwa ya akili yanaweza kumpata mtu yeyote, hivyo ni muhimu kuwafikisha katika vituo vya tiba watu wenaopatwa na matatizo hayo ili kuepusha madhara kwenye jamii yetu.

Monday, March 23, 2015

Harakati zangu kwenye mambo mbalimbali


Nilipata nafasi ya kuongozana na team nzima ya wanawakelive kwenda kufanya mahojiano na mshindi wa tuzo TWAA Jenifer Richard Shigoli, ambae alishinda  tuzo hiyo kupitia kipengele cha mwanamke mdogo mwenye mafanikio.
Hapa nilimuuliza baadhi ya maswali huyu shujaa wetu, kwa kweli nimejifumza mengi sana kupitia yeye. Alisema "Nilianza kutengeneza bidhaa zangu mwenyewe mara baada ya kumaliza Chuo kikuu Tumaini, ambapo bidhaa yangu ya kwanza niliitengeneza mwezi wa nane mwaka 2012. Nilianza kutengeneza bidhaa hizi za bulbby kwa mtaji wa shilingi elfu 23.
Hapa alinielezea kuhusu jinsi anavyofanya kufanikisha uuzaji wa bidhaa zake ambapo alisema baada ya kukabiliana na changamoto ya masoko na wateja aliamua kuja ma njia mbadala ya kukabiliana na changamoto hiyo ambayo ni kuanzisha kampeni ya Choo salama ambayo inajihusisha na kuisaidia jamii, mashuleni hasa shule za msingi katika kufanya usafi na pia kuwasambazia hizo bidhaa zake kwa nusu gharama. 

Saturday, March 14, 2015

Penye nia pana njia



Maisha ni vile  unavyoyataka yawe, ni vile unavyoyapigania na kuweka misimamo  thabiti na uwajibikaji. Chochote kile ambacho binadamu anaweza kukifikiria iwapo atakiamini na kukifanyia kazi kwa kujituma  bila kukata tamaa basi anaweza kukitimiza. Nilianza kuwa na ndoto za kufanya kazi kwenye runinga mwaka 2003 nikiwa darasa la nne. kwa wakati huo nilipenda kutangaza kipindi cha watoto ITV. Nilishiriki kwenye shindano la kutafuta mtangazaji wa kipindi cha watoto ITV lakini sikubahatika na licha ya hali hiyo sikukata tamaa niliamini siku moja nitatimiza lengo langu ilo.

Kwa kipindi hicho nilikuwa nikiimba na kuandika ngonjera, na mwaka 2004 nilirekodi nyimbo ambayo haikufanikiwa kuhit. Hata hivyo sikukata tamaa, nilishiriki kwenye mambo mbalimbali likiwemo Andika competition 2012 na kubahatika kuwa mshindni wa pili category politics(siasa) and economy(uchumi), n.k. Kuanzia 2011 nilikuwa nikitamani kumiliki kampuni yangu, na bado jitihada hizo zinaendelea. Lakini pia mwaka 2014 nilibahatika kupata nafasi ya kufanya kazi na Joyce Kiria (super woman) ambapo nafanya kazi mpaka ninapoandika hii post na nimeweza kujifunza vitu vingi na naendelea kujifunza kupitia yeye, hii yote ni kwasababu ya nia na malengo niliyonayo. Bado sijafika hata robo ya malengo yangu likiwemo la Kampuni, na hayo ni machache kati ya mengi ambayo nimewahi kuyafanya tangu kujitambua kwangu. Licha ya changamoto ninazokumbana nazo kila siku, bado napambana na huwenda mwaka huu nikatekeleza mipango yangu mingi zaidi. Penye nia, pana njia na nina imani malengo yangu yatatimia tu siku moja!!!